Nazunguka hata napaa
Huku na kule nakaa
Nikiwaaga marafiki
Wajane waso manafiki
Warembo wa vitendo
Na mayatima wa kiakademia
Wao watakaosalia nanga ning'oapo
New York mjini hakunitoshi
Atlantic City mradi nielekee
Ila tu maCasino siingii
Itanikoma basi nauli
Kwani 'Ujaluoni' nako hakusalii kamwe
Washington DC kuingia
Kaka Barry kumgotea basi ni lazima
Kwaheri na makumbatio
Machozi na mate ya tamati
yote siyapendi
Duniya tu ni barabara bali
Maisha hii kweli i safari
Mwendo wa kasi hapo awali
Sasa keshaingia tamati
Kujikokota tena siwezi
Ila bado fursa sipati
Na kusindikizwa kwa ajabu
Kweli raha ama huku tena hawanitaki
Mahenge tuandamane hadi Dubai
Daudi Nairobi ndiyo kikomo
Mtasemaje mlosema sitarudi?
No comments:
Post a Comment